Ijumaa , 21st Aug , 2020

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Kanda ya Dar es salaam Marison Mwakyoma amewataka madereva wa vyombo vya moto kuhakikisha wanaendesha vyombo hivyo kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.

Pichani Mkuu kikosi cha cha usalama barabarani kanda ya Dar es salaam Marison Mwakyoma

Kamanda Mwakyoma ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya madereva yaliyofanyika kwa siku kumi ambapo amesisitiza suala la sheria kutopindishwa kwa namna yoyote pamoja na kutoa wito kwa madereva hao kutotumika vibaya kisiasa.

"Kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kufanya uchaguzi mkuu madereva wanapaswa kuacha mihemko hasa kampeni za uchaguzi mkuu zitakapoanza" alisema kamanda Marison Mwakyoma

Katika mafunzo hayo ya siku kumi miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na mikakati muhimu ya kutambua maslahi ya kazi, sheria za usalama barabarani, kupokezana madereva kwa wale wanaosafiri masafa marefu pamoja na udhibiti uvunjaji hovyo wa sheria barabarani.