Ijumaa , 26th Jun , 2020

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ameagiza kuchukuliwa hatua kwa baadhi ya makampuni yanayojishugulisha na utafiti na uchimbaji wa madini pamoja na Gesi asilia ambayo yameshindwa kutoa mrejesho licha ya kupewa wito wa kufika katika kikao muhimu cha wadau wa madini.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko

Waziri Biteko ametoa rai hiyo wakati akizindua Kamati ya Taasisi ya uhamasishaji na uwajibikaji katika Rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini Tanzania.

Amesema katika kufanya tafiti mbalimbali, watafiti wa ndani wamefanya kazi kubwa na gharama nafuu hivyo haina budi kuthamini mchango mkubwa wanaofanya katika sekta hii. Aidha amesisitiza taasisi hiyo pamoja na Makampuni hayo yameanzishwa kwa mujibu sheria, hivyo ni wajibu kufuata taratibu.

Mhe. Biteko amesema ana imani na taasisi hiyo ya TEITA kutokana na wataalam walioko ndani ambao wamefanya kazi kubwa tangu kuanzishwa kwake.