
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Samia amewataka watanzania kuilinda minara hiyo ili iweze kuleta tija na kurahisisha mawasiliano nchini
"Mambo ya kwenda kuchimba udongo na michanga karibu na minara hii ilipo hayatatupeleka mbali, mambo ya kufanya hujuma mbalimbali kwenye minara hii ni kwenda kuhujumu maendeleo tunayoyapeleka vijijini" amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amewataka wasimamizi wa minara hiyo kuhakikisha kuwa umeme unakuwepo kwa kuwa ndipo itasaidia kushusha gharama za mabando
"Tukipeleka umeme tutatoa gharama ya kufanya kazi mnara mmoja kutoka milioni 1 na laki nane hadi laki nne hapo bando nalo litashuka tu kwa lazima, lisiposhuka tutajua jinsi ya kukamatana na watoa huduma hapa" amesisitiza Rais Samia