Jumapili , 28th Feb , 2021

Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameridhia na kumuidhinisha Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo Dr Peter Mathuki ambaye pia ameapishwa hii leo.

Katibu mkuu huyo Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Liberati Mfumukeko ambaye anatarajiwa kukabidhi ofisi mwezi April Mwaka huu kwa Dr Peter Mathuki.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi ameelezea pia teuzi nyingine za Majaji zilizofanyika hii leo ambapo Jaji Yohane Bakobora Masara wa Tanzania ameteuliwa kuwa jaji kiongozi wa mahakama ya haki ya Afrika Mashariki katika ngazi ya awali.

Pia Wakuu hao wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameidhinisha lugha ya Kiingereza,Kiswahili na Kifaransa kuwa lugh rasmi ya Jumuiya hiyo ambapo pia wameitaka sekretarieti ya Jumuiya hiyo kuendelea na mchakato wa kuridhia ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na jumuiya hiyo.
 

Tazama Video hapa