Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato
Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 2, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato, wakati akitoa ufafanuzi kufuatia changamoto ya ukatikaji wa umeme inayoendelea nchini.
"Tunayo changamoto kidogo ya upungufu wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme hasa kwenye maji, hilo limepelekea baadhi ya maeneo kukatika umeme au kupewa umeme kwa vipindi tofauti , serikali imeji-commit kabla ya mwezi unaokuja kuisha mradi wetu wa Kinyerezi 1 Extension utakaotupatia megawati 185 umekamilika ili kuondoa matatizo ya kukatika katika umeme," amesema Naibu Waziri Byabato