Jumatatu , 18th Jan , 2016

Kaya 437 zilizoathirika na mvua mkoani Mara zahitaji msaada wa chakula na pembejeo.

Serikali imeombwa kupeleka haraka msaada wa pembejeo za kilimo kwa kaya zaidi ya 437 katika kijiji cha Kasaunga kata ya Kisorya wilayani Bunda mkoani Mara ambazo mashamba yao zaidi ya ekari elfu mbili yamesombwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji hicho.

Mbunge wa jimbo la Mwibara mh Kangi Lugola, akizungumza baada ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko hayo amesema maafa hayo hayajawahi kutokea katika eneo hilo, hivyo kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kutoa msaada huo wa pambejeo .

Lugola ambaye pia ameambatana na baadhi ya viongozi wa serikali wa wilaya na mkoa wa Mara akiwemo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu mh Jenesta Mhagama, pamoja na mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Ester Bulaya, amesema waathirika hao pia wanahitaji msaada wa chakula.

Kwa upande Waziri Jenista Mhagama ameahidi kuongeza msaada wa chakula kwa wakazi hao