
Hery Mkunda, Katibu Mkuu TUCTA
Mkunda ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2022 wakati wa hotuba yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hizo za siku ya wafanyakazi ambayo yamefanyika kitaifa mkoni Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.
Mkunda amesema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzitekeleza hoja mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo punguzo la makato ya kodi, kupandisha madaraja, bado TUCTA inapendekeza kuongezewa mishahara walau shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini.
"Kauli yako ya 2021 ulisema 'Mimi ni Mama, na Mama ni mlezi', hivyo mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ile ahadi uliyotoa kuhusu kutupandishia mishahara wafanyakazi wote Tanzania, mishahara walau iwe shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini. TUCTA tunapendekeza, bila shaka hotuba yako leo itakuwa tiba sahihi"- Hery Mkunda, Katibu Mkuu - TUCTA