Alhamisi , 20th Aug , 2015

Ugonjwa wa kipindupindu bado unaendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo hadi kufikia leo kulikuwa na wagonjwa 38, ambao wamelazwa katika kambi maalumu za Mwananyamala na Mburahati.

Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala wakitoa matibabu kwa wagonjwa wa kipindupindu.

Kwa mujibu wa takwimu za kambi hizo, Hospitali ya Mwanayamala kulikuwa na wagonjwa 19 na Zahanati ya Mburahati wagonjwa 19, ambao wametokea maeneo mbalimbali ya Kinondoni, Manzese, Mburahati, Kimara, Mwenge na Mikocheni A.

Hapo jana Mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine watatu wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa morogoro ambao kati yao watatu ni familia moja na mmoja ni familia nyingine.

Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya amethibitisha kuingia kwa ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo nakuwataka wananchi kuchukua tahadhari katika ulaji wa vyakula na unywaji wa Maji.

Nao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu ugonjwa huo hatari na wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi wake pamoja na kutafuta vitendea kazi hasa kwa watu wanao fanya kazi za kuzoa taka na kuhakikisha mji unasafishwa ili kujikinga na ugonjwa huo.