Jumatano , 14th Mei , 2014

Kongamano la uwezeshaji kibiashara kwa nchi changa kiuchumi barani Afrika umeanza kufanyika leo jijini Mwanza.

Picha ya Pamoja ya Wajumbe na Viongozi wakuu wa Kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa linalofanyika Mkoani Mwanza, Mei 16 hadi 16, 2014

Kongamano la uwezeshaji kibiashara kwa nchi changa kiuchumi barani Afrika umeanza kufanyika leo jijini Mwanza.

Kongamano hilo limefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo kwa niaba ya waziri wa viwanda na biashara Dkt Abdallah Kigoda na litamalizika 16 mwezi huu.

Lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto na mustakabali wa nchi hizo ambazo zinashiriki kongamano hilo.

Katika hotuba yake Dkt Kigoda amesema Mkutano huu utakuwa chachu za kuinua viwanda vingi ambavyo vilikuwa vinafanya kazi wakati wa awamu ya kwanza kabla ya kufa na kupoteza mapato kwa serikali pamoja na ajira kwa wananchi.

Dkt kigoda ameziomba nchi mbalimbali zilizohudhuria kongamano hilo pamoja na mashirika ya kimataifa likiwemo shirika la biashara duniani WTO kuisaidia Tanzania kufufa viwanda vyake vya zamani pamoja kuboresha matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi.