Ijumaa , 4th Sep , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya kikwete amesema kuwa mipango mingi ya Serikali haifanikiwi kwa sababu ya kukosa Takwimu sahihi.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya kikwete

Dkt. Kikwete ameyasema hayo leo jijini Dar es salam wakati akifungua mkutano wa Afrika wa Takwimu huria uliowashirikisha Washiriki mia tano toka mataifa zaidi ya 30 toka Africa, Ulaya na Marekani.

Rais kikwete ameongeza kuwa nchi yoyote haiwezi kuendelea bila kuwa na Takwimu sahihi kama hakuna wataalamu wa kutosha wa kuzikusanya takwimu hizo, teknolojia ya kisasa na miundombinu hafifu.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Benk ya Dunia hapa nchini Bella Bird amesema katika nyakati hizi takwimu huria ambazo kila mtu ataweza kuzifikia ni nyenzo muhimu sana katika kuleta maendeleo ya haraka duniani hasa Afrika ambapo matumizi ya takwimu sahihi ni madogo kulinganisha na Ulaya na Marekani.