Jumapili , 8th Dec , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepongeza hatua kuanza kwa safari za treni kuelekea mkoani Moshi, baada ya miaka 25, ambapo amesema hatua ni kubwa sana iliyofanywa na Shirika la Reli Tanzania TRC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akiwa kwenye Uzinduzi wa Uwekaji wa mawe ya msingi ya ujenzi wa Meli na Chelezo katika Miradi Ziwa Victoria.

Rais Magufuli amesema kuwa "Bada ya miaka 26 ndiyo Meli imeanza kwenda Moshi, Wakati wa Mwalimu Nyerere treni ilikuwa inaenda Moshi, alivyokuja Mwinyi 'Ikastop', tungejiuliza Why, lakini tumeamua leo Treni inaenda huko, sio kwamba tulikuwa hatuna hela ila hatukuweka kipaumbele"

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa "Wakati wa Uchaguzi niliahidi kununua meli, na sikujua hela naitoa wapi na nikajiuliza ningeweza kweli, ila sasa kupitia Watanzania sasa tumeweza"