Jumatatu , 21st Jan , 2019

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchi, Ahmed Msangi amesema lolote linaweza kutokea kwenye ofisi ya IGP baada ya utenguzi uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Kangi Lugola.

Insipekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro

Kamanda Msangi amesema hayo leo wakati akijibu swali kuhusu kuendelea kuwepo ofisini kwa Wakuu watatu wa polisi wa mikoa mitatu tofauti waliotenguliwa na Waziri Lugola wiki iliyopita.

"Utenguzi aloufanya waziri Lugola suala kwenye meza ya ya Insipekta Jenerali wa Jeshi la polisi, hivyo lolote linaweza kutokea", amesema Kamanda Msangi.

Jumamosi hii, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, akizungumzia kuhusu Makamanda aliowatumbua kuendelea na kazi alisema kwamba yeye alishatoa maagizo ya kuondolewa kwenye nafasi zao kwa Makamanda wa Polisi watatu katika Mikoa mitatu ya kipolisi Temeke, Ilala pamoja na Arusha na kilichobaki ni kutekelezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kangi Lugola alitoa uamuzi huo wa kutengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu akiwemo Salum Hamduni aliyekuwa Ilala, Emmanuel Lukula (Temeke) kwa kosa la kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.