Lowassa ataka mazungumzo Zanzibar yaongeze wadau

Ijumaa , 15th Jan , 2016

Waziri Mkuu wa Zamani na Aliyekua Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa ametaka kupanuliwa kwa wigo wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Waziri Mkuu wa Zamani na Aliekua Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam Mhe. Lowassa ameshauri katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ni vyema wadau mbalimbali wakahusishwa nje ya vyama vinavyokinzana vya CCM na CUF

Mhe. Lowassa amesema mgogoro huo hauwezi kupata ufumbuzi wa haraka endapo vyama hivyo viwili vitaendelea na mazungumzo kwa kuwa kila chama kinavutia upande wake hivyo kufanya mazungumzo hayo kutokufikia muafaka.

Aidha katika hatua nyingine amekitaka Chama cha Mapinduzi kuomba radhi kupitia kiongozi mkubwa wa chama hicho kuhusu kauli ya kibaguzi iliyoandikwa katika moja ya mabango yaliypitishwa siku ya sherehe ya mapinduzi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu huyo wa Zamani amesema kueleka uchaguzi wa mwaka 2020 serikali haina budi kukubali kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ili kuondoa malalamiko ambayo yanasababisha uchaguzi kuingia na dosari.