Jumatatu , 29th Jun , 2015

Utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), unamtaja Mbunge wa Monduli nchini Tanzania Edward Lowassa kuongoza katika kutaja vipaumbele vya maendeleo kati ya watia nia wa nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi CCM.

Baadhi ya Wagombe waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais kwa chama cha Mapinduzi, CCM,

Akizindua ripoti hiyo mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Kateri,amesema miongoni mwa vipaumbele vilivyompa alama kubwa ni pamoja na sera ya kupunguza tatizo la Ajira nchini na kuinua Elimu,

Kateri ameongeza kuwa ripoti hiyo imejumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini ambapo kipengele cha watangaza nia walioshuhudiwa na watu wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa kushuhudiwa kwa asilimia 54, akifuatiwa na Bernard Membe (46%) Mwigulu Nchemba (44%) Steven Wasira (40%), Jaji Augustino Ramadhani (39%) , na wengi ni na wengine wakifuata..

Wilaya zilifanyiwa utafiti huo ni Kinondoni,Kibaha Vijijini,Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu, na Babati, Lindi,Mtwara, Njombe Mjini, Njombe Vijijini, Mbeya mjini, Nyamagana, Biharamulo, Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino. Na Kasulu.