Jumamosi , 25th Mei , 2019

Sakata la watuhumiwa 17 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo unyang’anyi, mauaji na uhujumu uchumi, waliotoroka katika mazingira ya kutatanisha limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola kuibuka mkoani humo.

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola

Akiwa mkoani Geita Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amefikia maamuzi ya kuwasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya, Mkuu wa Kituo cha Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Wilaya hiyo, na kuagiza askari waliotorokwa na watuhumiwa kukamatwa mara moja.

Waziri Lugola alipowasili kabla ya kutoa uamuzi huo alifanya kikao na kamati za ulinzi na usalama wilaya na Mkoa, pamoja na kutembelea kituo cha polisi wilaya , Magereza na baadaye eneo ambalo mahabusu hao waliwatoroka.

"Jambo hili limenisikitisha sana, mahali ambapo kuna viongozi wajuu wa polisi, ambapo Maaskari hao wamesababisha tukio hili kana kwamba hakuna kilichotokea, nimeelekeza RPC hao Maaskari hao waliohusika wakamatwe ni waharifu kama waharifu wengine." amesema Lugola

"Jambo hili Mkuu wa Mkoa lazima lichunguzwe kuona kiini chake kwa maelezo tuliyoyapata na kwakuwa viongozi hawa watatu wamechukua hatua za awali kwa hawa maaskari, natoa maelekezo kwa Katibu wa Mambo ya Ndani kuwasimamisha kazi OCD, na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Geita." amesema Lugola

ao waliokuwa wamehifadhiwa katika Ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita, kabla ya kuhamishiwa katika Ukumbi wa Jengo Jipya la Mahakama hiyo walitoroka mbali ya ulinzi wa askari zaidi ya watano waliokuwa wamezunguka jengo hilo,huku jeshi la polisi Mkoa likipata kigugumizi kuzungumzia tukio hilo.