Ijumaa , 19th Aug , 2022

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amesema kwamba  maandamano ya wiki iliyopita dhidi ya serikali yake yalikua ya kushtukiza na kupelekea  Polisi kutumia nguvu nyingi

Maandamano hayo yalipelekea vifo vya watu takribani 25 wakiwemo Askari Polisi 5

Raia wa nchi hiyo walikua wanaandamana wakipinga maisha kuwa magumu, rushwa na ukatili wa polisi wa nchi hiyo 

Rais Julius Maada Bio  amesema kuwa licha ya baadhi ya askari polisi kutokua na weledi lakini maandamano hayo yalikuja kwa kushtusha na kupeleka nguvu nyingi kutumika

Rais  Bio ameulaumu upinzani    wan chi hiyo kwa kujaribu kuitikisa serikali yake , madai ambayo yanapingwa na upinzani wa nchi hiyo  

Ameongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua ukweli wa maandamano hayo 

Amesema baadhi ya waandamanaji walikua wanawachochea watu kufanya mauaji na kuwashinikiza wanajeshi kuingia ikulu ya nchi hiyo 

Rais huyo ametetea maamuzi yake ya kufanya mabadiliko kwenye jeshi la nchi hiyo baada ya maandamano hayo huku akikanusha tishio la kupinduliwa