
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto
Kamanda Muroto ameyabainisha hayo leo Septemba 5, Jijini Dodoma na kusema kuwa wakati wabunge wakilalamikia kukithiri kwa machangudoa mkoani humo, Jeshi la Polisi mkoani humo lilikuwa limekwishaanza kuchukua hatua muda mrefu tu.
''Ni kweli machangudoa wapo, lakini watuhumiwa hawa wanadhibitiwa tumeshawakamata takribani makahaba 15 tukawafikisha Mahakama ya Makole na wamefungwa miezi 6, sasa hawa madada poa, badala ya kuwa dada poa watakuwa wameangukia pua, Kwahiyo Gereza la Isanga wawapokee kwa ajili ya nguvu kazi wakapige mawe badala ya kuishi wakitegemea kuuza miili yao'' amesema RPC Muroto.
Aidha Kamanda Muroto ameongeza kuwa Jeshi la polisi mkoani humo, linaendelea na msako, ambao hautakuwa na kikomo na kuwataka wale wote wanaoenda kutafuta fursa ya ngono mkoani humo wajue nafasi hiyo haipo.