Jumanne , 26th Dec , 2017

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amewataka wamiliki wa magari wanaofanya safari ndefu kuhakikisha kunauwepo wa madereva wawli.

Kamanda Shanna amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza ajali katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwani kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huwa kunakuwa na ajili nyingi huku akitaja chanzo chake kinakuwa ni uzembe wa madereva.

Aidha kamanda Shanna amewataka madereva ambao sio wazoefu wa kuendesha magari ya abiria wasiendeshe na badala yake kuwatafuta madereva walio wazoefu ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Katika taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi Mkoani Pwani inaonyesha kuanzia January ya mwaka huu hadi mwanzoni mwa  Desemba, 2017 matukio ya ajali yamepungua kutoka 396 mwaka jana hadi kufika 98.