Jumatatu , 29th Mar , 2021

Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe unatarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma zote za afya kuanzia Julai 1, 2021.

Hospitali ya wilaya ya Wanging'ombe

Hospitali hiyo ni miongoni mwa takribani hospitali 70 za wilaya zinazoendelea kujengwa nchini kwa maelekezo ya aliyekuwa Rais Hayati Dk. John Magufuli.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amesema Hayati Dk. Magufuli ataendelea kuenziwa wilayani humo kwa kukamilisha miradi mikubwa ikiwemo hospitali hiyo ya wilaya ambayo itakwenda kuwasaidia sana wananchi.

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Wanging'ombe

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Dk. Girliad Lupembe ni amesema katika kipindi cha miaka mitano ya Dk. Magufuli amefanikisha kupatikana kwa hospitali ya wilaya na tayari fedha za kukamilisha wodi mbalimbali zimeshaletwa na zinaendelea kujengwa.