
Mbunge wa Juja nchini Kenya George Koimburi, alivyokutwa shambani
Kwa mujibu wa video fupi za CCTV zilionesha mbunge huyo alichukuliwa kwa nguvu na watu hao wasiojulikana na kuondoka naye wakitumia gari aina ya Subaru Forester yenye rangi ya silver, huku mke wake akiachwa na majeraha kutokana na purukushani hizo.
Idara ya Upepelezi na Makosa ya Jinai nchini Kenya imekana kuhusika na tukio hilo, licha ya kuthibitishwa kwamba mbunge huyo amekuwa akitafutwa tangu Ijumaa kuhusiana na matukio ya udanganyifu wa ardhi na matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa jimbo.