Jumatano , 25th Jan , 2023

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Jerry Muro, amepigwa chini kwenye nafasi hiyo kufuatia uteuzi uliofanywa hii leo Januari 25, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jerry Muro

Nafasi ya Jerry Muro imechukuliwa na Thomas Cornel Apson, ambaye hapo awali alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Siha.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteua wakuu wa wilaya wapya 37 huku 55 wakibaki kwenye wilaya zao na wengine 48 wamehamishwa wilaya. Idadi hiyo inafanya kuwa jumla yao kuwa wakuu wa wilaya 140 ambapo kati yao wanaume ni 100 na wanawake ni 40.