Ijumaa , 24th Feb , 2023

Msichana mwenye umri wa miaka 11 nchini Cambodia amefariki sababu ya mafua ya ndege, ikiwa ni  kisa cha kwanza cha binadamu kinachojulikana nchini humo cha homa ya ndege katika kipindi cha miaka tisa,

 

 

mamlaka za afya nchini humo  zimethibitisha kifo hicho,ambapo  msichana huyo kutoka jimbo la Prey Veng vijijini alipatikana na virusi vya H5N1 siku ya Jumatano.

Taarifa zinasema msichana huyo alikuwa ameugua kwa wiki moja ambapo alipatwa na  homa kali, kikohozi na maumivu ya koo.

Wizara ya afya ya Cambodia imesema baba yake pia alipimwa na wengine 11 wamepimwa.

Hii leo , Waziri wa Afya Mam Bunheng amesema ni maambukizi ya kwanza ya binadamu yanayojulikana ya aina ya H5N1 nchini Cambodia tangu 2014.Msichana huyo alikuwa amechukuliwa kutoka kijijini kwake hadi hospitali ya watoto katika mji mkuu Phnom Penh  lakini alifariki muda mfupi baada ya kugundulika.