Jumapili , 20th Mar , 2016

Katika kuadhimisha kilele cha siku ya afya ya kinywa na meno Duniani iliyoadhimishwa kitaifa Mkoa

Katika kuadhimisha kilele cha siku ya afya ya kinywa na meno Duniani iliyoadhimishwa kitaifa Mkoani Morogoro baadhi ya wakazi wa mji huo wamemeshauri Chama cha Madaktari wa Meno nchini kuendelea kutoa huduma hizo mara kwa mara katika maeneo ya vijijini kufuatia wananchi wengi kushindwa kufika mjini kwa lengo la kupata huduma hizo.

Wakizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya kinywa na meno duniani wananchi hao wameeleza kufurahishwa na huduma hizo ambapo wamesema ni vyema uwepo utaratibu wa kutoa huduma hizo mara tatu kwa mwaka ili wananchi wapate fursa ya kuelewa namna ya kutunza kinywa na meno yao kinywa.

Akitoa tarifa ya zoezi la utoaji huduma ya afya ya kinywa na meno katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro mkuu wa idara ya kinga ya kinywa na meno hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dokta Baraka Nzobo amesema idadi kubwa ya watoto wanakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa meno na fizi.

Ameeleza kuwa katika watoto 271 jumla ya watoto 174 walikutwa na matatizo ya ugonjwa wa kinywa hivyo kutengeneza asilimia 62, na kuwa tatizo hilo ni kubwa huku akieleza asilimia 37 walikutwa na meno yalioooza na 18 wengine magonjwa ya fizi na asilimia walikutwa na magonjwa mengine ya kinywa na meno.