Alhamisi , 12th Sep , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua na kumuapisha Kamishna Diwani Athumani Msuya, kwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Rais Magufuli (kushoto) na Diwani Athumani akila kiapo (kulia).

 

Rais Magufuli (kulia) katika picha ya pamoja na Diwani Athumani (kushoto).

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Diwani Athumani amechukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba, ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Uteuzi huo umeanza leo Septemba 12, 2019, kama inavyoeleza zaidi taarifa hapo chini.