Ijumaa , 11th Sep , 2015

Kampeni za kuwania Urais kupita vyama mbalimbali nchini zimeendelea jana huku wapinzani wawili wakubwa wakinyanganyiro hicho wakiendelea na mikutano yao katika mikoa tofauti

Mgombea Urais wa kupitia CCM John Pombe Magufuli na Mgombea Urais kupita UKAWA Mh. Edward Lowassa

Mgombea Urais wa kupitia CCM John Pombe Magufuli yeye alifanya ziara ya kuzunguka baadhi ya vijijini mkoani Mara na mgombea Urais kupita UKAWA Mh. Edward Lowassa alikuwa Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.

Akiwa Mkoani Mara Wilayani Bunda Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mh. John Pombe Magufuli alisema serikali yake kamwe haitavumilia viongozi wazembe ikiwemo kuwawajibisha watakabainika kuacha kutumia fedha za miradi ya maendeleo ipasavyo.

Aidha Mh. Magufuli ameongeza kuwa asipohubiri amani katika mikutano yake basi atakuwa amekosa sifa za Urais hivyo ameahidi kuhubiri amani ya nchi kwenye kila mkutano atakoufanya.

Kwa upande wake mgombea wa Urais wa UKAWA kupita chama cha Demokrasia na Maendele CHADEMA Mh. Edward Lowassa akiwa mkoani Morogoro wilayani Gairo amesema endapo akiingia madarakani atatatua suala la Uhaba wa maji katika wilaya hiyo.

Mh. Lowassa amewataka wakazi wa mkoa huo wamchague mbunge ambaye ataweza kufanya naye kazi ili kuweza kutatua kero nyingine mbalimbali zinazowakabili wakazi wa eneo hilo.