Alhamisi , 2nd Jan , 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, leo Januari 2, 2020 imekataa ombi la Mwandishi wa habari Erick Kabendera, kushiriki katika ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi Verdiana Mjwahuzi aliyeaga dunia Disemba 31, 2019, yatakayofanyika Januari 3, mwaka huu, Kanisa Katoliki.

Hali ya Kabendera leo Januari 2, 2020, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

la Chang'ombe, lililopo katika Wilaya ya Temeke.

Maombi hayo yaliwasilishwa na mawakili wake wakiongozwa na Jebra Kambole, mbele ya Hakimu Janet Mtega wa Mahakama hiyo.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alitoa pole kwa Erick kufiwa na mama yake ambapo licha ya pole hizo, upande wa mashtaka ulitupilia mbali ombi hilo kwa madai ya kuwa hoja za upande wa utetezi hazikuwa na mashiko.

Erick Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa pesa pamoja na ukwepaji wa kodi ya zaidi ya Shilingi milioni 170, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.