Jumanne , 10th Sep , 2019

Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo ameongezewa kifungo kutoka miezi mitano jela hadi mwaka mmoja.

Baba levo (katikati)

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 10, 2019 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, baaada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali. 

Baba Levo alikata rufaa katika mahakama hiyo kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia trafiki, F.8350 PC Msafiri Mponela.

Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.