Jumatano , 13th Oct , 2021

Jana Oktoba 12, 2021, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alishiriki sala fupi ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye kaburi lake wilayani Chato, mkoani Geita.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliposhiriki ibada fupi ya kumuombea Hayati Dkt. John Magufuli

Wengine walioshiriki kwenye sala ile ni Mama Janeth Magufuli, Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, na wengineo.