Mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi ya leo asubuhi yanakuja wakati ambapo maafisa wa KDF na GSU wanapambana katika eneo hilo kuwaondoa majambazi.Marehemu ni pamoja na mkuu wa chifu wa eneo hilo na wananchi wawili katika mkoa huo.
Miili ya waathiriwa hao watatu ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kaunti ya Samburu ikisubiri kufanyiwa uchunguzi baada ya kifo. Wenyeji walisema majambazi hao kutoka jamii jirani walivamia zaidi ya vijiji vitatu na kuswaga mamia ya mifugo.
Polisi wamesema kwamba baadhi ya maafisa wa usalama walipata majeraha ya risasi wakati wakirushiana risasi na majambazi hao.
"Tulishambuliwa na majambazi asubuhi. Sasa hatuna matumaini kwa sababu ikiwa jeshi haliwezi kuwazuia watu hawa, basi ni nani?" alihoji Jackson Lanyasunya, Mkazi wa wa eneo hilo.





.jpg?itok=5cvL0YaP)