
Mwanaume aliyeleta taharuki jana na kusababisha mauaji ya watu wanne
Majirani hao akiwemo Said, Omary na Issa, wameyasema hayo leo Agosti 26, 2021, wakati wakizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, na kuongeza kwamba wameshangazwa na tukio hilo.
"Hamza hakuwa mzungumzaji kwa sana, hana matatizo na mtu yoyote nimeshangaa sana kwa lile tukio, ukikaa naye ni mtu wa kawaida sema hana mazungumzo mengi," amesema Said, ambaye ni jirani yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi hapo jana, jumla ya watu wanne walipoteza maisha, wakiwemo Askari watatu na mmoja kutoka kampuni binafsi ya ulinzi katika tukio hilo lililozua taharuki karibu na ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam.
Aidha, Jeshi la Polisi, tayari limeweka ulinzi katika nyumba aliyokuwa akiishi Hamza iliyopo maeneo ya Upanga na waliwachukua ndugu zake kwa ajili ya mahojiano.