Jumamosi , 26th Feb , 2022

Mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza Salum Kali, amesema bado wanaendelea kuwatafuta waliobomoa na kuiba baadhi ya vitu kama misalaba na baadhi ya viungo vya miili ya watu waliozikwa kwenye makaburi ya wilaya hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Moja ya kaburi lililobomolewa

Kauli hiyo ameitoa wakati wa zoezi la usafi lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo kwenye makaburi ya wilaya ambayo mengine yamebomolewa na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa, hadi sasa watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kubomoa makaburi hayo na kuiba misalaba pamoja na baadhi ya viungo vya miili iliyozikwa hapo na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.