Jumanne , 3rd Mei , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla, amaetoa Muda wa wiki moja kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Kanda ya Mbeya, kumchukulia hatua za kinidhamu muuguzi aliedaiwa kumpiga Mzazi Salome Waya, wakati wa Kujifungua.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla,

Makalla ametoa muda huo mara badaa ya kufanya ziara ya kushtukiza katika katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, kitengo cha wazazi cha Meta ambapo ndipo alipokutana na shutuma hizo.

Licha ya kukutana na msongamano katika wodi hizo ambapo wazazi wanalala wawili wawili huku akiadi kushungulikia lakini katika wodi namba mbili ndio amekutana na malalamiko ya mama huyo Salome Waya.

kutokana na hatua hiyo Mkuu wa Mkoa aliamua kufuatilia tukio hilo na ndipo alipomuagiza Mkurugenzi wa Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kuunda tume ya kuuchunguza tukio hilo ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi huyo wa Hospitali hiyo Dkt. Godlove Mbwaji, amesema kuwa ataunda tume huru ya kuchunguza jambo hilo ambayo itajumuisha wananchi pamoja na idara ya serikali ya wilaya na hospitali hiyo ili kubaini tatizo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla na Mkurugenzi huyo wa Hospitali hiyo Dkt. Godlove Mbwaji wakiongelea tukio hilo
Sauti ya Salome Waya Mazazi anaelalamikia kupigwa wakati akijifungua