Ijumaa , 16th Nov , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameambatana na , Meya wa jiji, Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye Stand Mpya ya Mabasi ya Msamvu kujifunza namna ilivyofanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa na Meya wa jiji hilo Isaya Mwita pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa.

RC Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa stand Mpya ya kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi billion 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa Mara nne ya Stand ya Msamvu ambapo itakuwa na uwezo wa kupokea Mabasi 500 kwa wakati mmoja.

Aidha RC Makonda amesema Stand mpya ya Mbezi Luis itakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel,Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo,kituo cha polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.

Pamoja na hayo RC Makonda ameonyesha kufurajishwa na namna stand ya Msavu ilivyoweza kuweka utaratibu mzuri kiasi cha kuongeza mapato kutoka shilingi 350,000 hadi kufikia Shilingi Million 4.5 kwa Siku.

Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na wamesema watafika Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani Na nje ya nchi.