Paul Makonda
Wakili huyo aliyejitambulisha kama Goodchance Regnald ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Aron Ryamuya katika kesi ya maombi ya kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya Paul Makonda, DPP na DCI katika mahakama hiyo.
Wakili Goodchance ameongeza kwa kusema kuwa Makonda hakupata hati rasmi ya wito zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, na hivyo akaamua kumtuma wakili wake kuja mahakamani.
Baada ya Wakili Goodchance kueleza hayo akaiomba Mahakama kumpa hati hiyo ya wito ambayo mteja wake ataijibu, jambo ambali Hakimu Ryamuya aliamuru kufanyika leo.




