Jumatano , 13th Mar , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema anataka mpaka kufikia Uchaguzi Mkuu 2019/2020 wakazi wa Jiji la Dar es salaam wakiwa wanashiriki zoezi hilo la kuchagua viongozi wakiwa hawana ugonjwa wa tezi dume.

Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda

Paul Makonda ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam ambapo amesema nia yake kama Mkuu wa Mkoa ni kuhakikisha wananchi wa Mkoa wake wakiwemo wanaume na wanawake wanapima ugonjwa tezi dume.

Makonda amesema, "nadhani mwaka huu ndiyo sahihi wa kuendesha zoezi la upimaji wa tezi dume, nataka wanaume na wanawake wote tunaenda uchaguzi wa 2019, 2020 hakuna tezi dume."

"Kama wewe ni mwananchi wa Dar es salaam na unaelekea Dodoma tutakufuata huko hatutaki uende mkoa mwingine ukiwa unaumwa, niwaombe wananchi wa Dar es salaam wajitokeze kupima na usipokuja tutakufuata nyumbani kwa sababu ni jukumu letu kukulinda", ameongeza Makonda.