Jumatatu , 17th Feb , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuzirudisha zile pesa za TASAF alizodai kupewa na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa mwaka 2012.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Hayo ameyabainisha leo Februari 17, 2020, wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, na kuzitaja changamoto zilizojitokeza katika zoezi la uhakiki wa Kaya maskini, lililofanyika 2015 hadi June 2017, ambapo zilibainika kaya hewa 73,561.

"Kaya 22,034 zilithibitika wanakaya wake siyo maskini na mojawapo ni akina Makonda ambao walizitumia fedha hizo kwenda Dodoma wakati siyo maskini na ninaomba kama hili ni ukweli Makonda azirudishe hizo fedha, kama kweli alituma fedha za TASAF lazima hizo fedha azirudishe" amesema Rais Magufuli.

Katika hotuba yake Makonda alieleza ni kwa namna gani Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, alivyompatia fedha za TASAF na kuzitumia kwenda nazo Dodoma kuomba ridhaa ya kuchaguliwa nafasi ya Makamu Mwenyeki wa UVCCM