Jumatano , 2nd Jul , 2025

Msimu mpya wa Ligi ya La Liga nchini Uhispania 2025/26 unatarajia kuanza tarehe 17 Agosti kwa michezo yote ya mzunguko wa kwanza kupigwa.

Mabingwa watetezi FC Barcelona wamepangwa kuanzia ugenini dhidi ya Mallorca huku wapinzani wao Real Madrid wataanzia nyumbani dhidi ya Osasuna wakati kikosi cha Atletico Madrid watakipiga ugenini dhidi ya Espanyol.

Michezo ya kuvutia ya El Clásico imepangwa kufanyika Oktoba 26 kwa Real Madrid kuanzia nyumbani huku mchezo wa mkondo wa pili utanyika Mei 10/2026 FC Barcelona wakiwa nyumbani.

Msimu uliopita Real Madrid walipoteza michezo yote miwili ndani ya La Liga (0-4 & 4-3) ukiitoa michezo mingine miwili waliopoteza Super Cup (2-5) na Copa del Rey (3-2) na kuwafanya Madrid kupoteza michezo minne kwa msimu mmoja dhidi ya Barca.