Jumanne , 16th Sep , 2025

Mutharika (85), kampeni zake zinadaiwa kujikita kwenye ahadi ya kufufua uchumi na kurejesha uongozi ambao anasema, umeyumba.

Raia wa Malawi, hivi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa rais, Wabunge na madiwani, uchaguzi ambao unatarajiwa kuamua mustakabali wa taifa hilo kuhusu uchumi na vita dhidi ya rushwa.

Rais wa sasa mchungaji Lazarus Chakwera na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Peter Mutharika wanachuana vikali kutika uchuguzi huo ambao una jumla ya wagombea 17 wanaotafuta uongozi wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Chakwera na Mutharika kupambana, kwenye kinyanganyiro cha kutafuta urais. Utawala wa Chakwera, umekumbwa na changamoto nyingi za kiuchumi na athari nyingi za mabadiliko ya tabia nchi hasa mafuriko lakini amekuwa akiomba kura, akiahidi kumalizia yale aliyoanzisha kama ujenzi wa barabara shule na hospitali.

Mutharika (85), kampeni zake zinadaiwa kujikita kwenye ahadi ya kufufua uchumi na kurejesha uongozi ambao anasema, umeyumba.

Hata hivyo, uwepo wa Dalitso Kabambe, aliyekuwa Gavana wa Benki kuu, anayetafuta uongozi wa nchi hiyo, unaelezwa huenda ukatatiza ushindi wa mzunguko wa kwanza, Septemba 16 na kupeleka uchaguzi huo kwenda kwenye mzunguko wa pili.