Jumatano , 17th Feb , 2016

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth Magufuli amesisitiza wazazi wawapeleke shule wanafunzi wenye umri wa kwenda shule kwani kwa hivi sasa elimu ni bure.

Ameyasema hayo hii leo wakati wa hafla ya kumuaga rasmi kama mwalimu wa shule hiyo hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Mbuyuni na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hiyo .

Mama Magufuli alisoma katika shule hiyo kuanzia darasa la kwanza na baaadaye mwaka 1995 kujiunga na shule hiyo kama mwalimu na kutumikia wadhifa huo mpaka alipokuwa mke wa Rais ambapo amelazika kuacha kuendelea kufundisha katika shule hiyo.