Mama Salma Kikwete akila kiapo bungeni
Katika swali lake Mama Salma Kikwete amehoji kuhusu mpango wa serikali kuongezea huduma ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) hasa watu masikini wakiwemo katika mkoa wake wa Lindi.
Akijibu hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema kuwa serikali imepanga katika mwaka wa fedha 2017/2018 kuandikisha kaya zote zilizobakia katika mpango huo na kwamba hadi sasa mpango huo umefikia asilimia 70 kwa nchi nzima huku ikiwa imebakiza vijiji 5,690 sawa na asilimi 30 ili kuweza kukamilisha mpango huo kwa asilimia 100.
Angela Kairuki - Waziri Utumishi na Utawala Bora
Mhe. Kairuki amesema jumla ya Kaya 355,000 zilizobakia zitaweza kutambuliwa pamoja na kuandikisha kaya masikini katika mikoa na vijiji vilivyobakia katika mpango huo.
Msikilize hapa chini mama Salma alipokuwa akiuliza swali la nyongeza..............................
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (katikati) alipohudhuria kuapishwa kwa mke wake , Mama Salma Kikwete Bungeni Dodoma