Jumatano , 5th Apr , 2023

Serikali kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC imewasimamisha kazi Mameneja wa Kampuni ya TANOIL – Kampuni Tanzu ya TPDC, inayojihusisha na biashara ya mafuta.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, kuashiria ubadhirifu mkubwa katika uendeshaji wa taasisi hiyo.

Waliosimamishwa ni Meneja Mkuu Kapuulya Musomba, Meneja wa Fedha na Utawala James Batamuzi, Meneja wa Hifadhi ya Mafuta Sudi Abdalla na Meneja wa Usambazaji na Uendeshaji Manager Amour Marine.

Soma taarifa kamili ya Wizara