Jumapili , 28th Sep , 2025

Baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege, mwili wa Askofu Rugambwa umepelekwa makao makuu ya Kanisa Kuu Katoliki Bukoba (Cathedral) huku ukisindikizwa na viongozi wakuu wa kanisa, viongozi wa Serikali pamoja na waumini.

Waumini wa Kanisa Katoliki mkoani Kagera wameupokea mwili wa Askofu Rugambwa, ambaye alikuwa ni Balozi wa Papa nchini New Zealand, katika uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuwasili kwa ndege majira ya saa 6:17 mchana kutokea jijini Dar es Salaam.

Ibada za kuupokea mwili huo zimeongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage zikifanyika katika uwanja wa ndege na pia katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma (Cathedral Bukoba) kwa ajili ya taratibu za mazishi kesho, Septemba 29, 2025.

Baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege, mwili wa Askofu Rugambwa umepelekwa makao makuu ya Kanisa Kuu Katoliki Bukoba (Cathedral) huku ukisindikizwa na viongozi wakuu wa kanisa, viongozi wa Serikali pamoja na waumini.

viongozi wengine walioshiriki katika mapokezi ya mwili huo ni pamoja na Askofu mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Desderius Rwoma, Askofu msaidizi mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini; Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi; Askofu msaidizi wa Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu; Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, Mhashamu Ludivick Minde; na Askofu wa Jimbo Katoliki Mbinga, Mhashamu Chrizostom Ndimbo.