Jumanne , 25th Aug , 2020

Katibu Mkuu Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya amesema Miradi mingi ya Elimu na sekta ya Afya inayoendelea kujengwa katika Manispaa ya Ilala inaonesha thamani halisi ya Pesa ilizopangiwa.

Katibu Mkuu Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT)kulia Elirehema Kaaya akiwa katika ukaguzi wa miradi.

Bw kaaya ametoa kauli hiyo Mara baada ya kufanya ziara  katika shule ya Kasulu inayojengwa madarasa ya ghorofa,kituo cha afya Buguruni ambapo ameridhishwa na Kasi ya ujenzi akiwataka watendaji wa Manispaa hiyo kuendelea kuongeza Kasi katika makusanyo ya Mapato ya ndani ili kuelekeza katika miradi yenye  manufaa kwa Wananchi.

 "Ujenzi Kama huu wa maghorofa uliofanywa na Manispaa ya  Ilala ni muhimu mno kwa kuwa unaweza kutumia eneo dogo kujenga majengo mengi zaidi hivyo nikupongeze Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Timu yako endeleeni kutekeleza ndoto za Serikali" alisema Elrehema Kaaya Katibu Mkuu ALAT.

Amesema kitendo cha kujenga jengo kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko eneo la kipawa  itaasaidia endapo itatokea majanga huku akizitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa kilichofanywa na Ilala katika kutumia eneo dogo kwa masilahi mapana.

Jengo hilililojenga kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko litawasaidia Wakazi wote wa Manispaa hii kwa mfano hivi karibuni tuu  nchi yetu imetoka kwenye janga la Covid 19 niseme ukweli katika majengo haya naiona thamani halisi ya pesa kwenye miradi hii endeleeni na Kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani"alisema Elirehema Kaaya-Katibu Mkuu ALAT.

Kwa miaka minne mfululizo Manispaa ya Ilala imekuwa ikipata hati Safi kutoka kwa Mkaguzi mkuu wa Serikali akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na watendaji kuendeleza mapambano ya kuwatumikia wananchi walio wanyonge ili kuinua Hali zao kwakuwa ndiyo kipaumbele Cha Serikali.