Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Katibu Mkuu wa Wizara ya ardhi Dkt Allan Kijazi amesema mapato ya ardhi yanayolipwa kupitia miamala mbalimbali bado yako chini huku zikitajwa baadhi ya changamoto kadhaa ikiwemo mifumo isiyo rafiki ya makusanyo ya mapato ya ardhi kutoka Kwa wananchi

Dkt Allan Kijazi amebainisha kuwa endapo Wizara itaweka mifumo ya makusanyo sawa inaweza kukusanya mara tatu zaidi ya lengo ambalo imejiwekea la Shilingi bilioni 200 ya Sasa

Hata hivyo amesema kikao Cha Leo kimewahusisha wadau ambao Wizara inawatumia wakiwemo kampuni za simu,benki na mawakala wao ambao wamesambaa maeneo mengi ikilenga kujadili kuongeza Kasi ya mapato Kwa kuwa imeonekana wananchi wengi wanamiliki ardhi bila kulipia chochote.

Amesisitiza kuwa zipo changamoto ambazo Wizara imelenga kuzitoa Kwa wananchi ikiwemo elimu, kufanya uwekezaji katika mifumo itakayo wafikia wananchi huko waliko Ili kuongeza Pato kutokana na Kodi za ardhi Ili kuzidi makusanyo ya asilimia 60 yaliyofikiwa mwaka 2021