Rais wa Marekani Joe Biden
Rais Biden ameongeza kuwa Urusi imekusudia kuingia katika vita ambayo itapoteza maisha ya watu na kuleta maafa na kwamba itawajibika kwa vifo vya watu na maafa yatakayotokea katika vita hiyo.
Kwa upande wake Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema hana lengo la kuichukua nchi ya Ukraine katika oparesheni hiyo ya kijeshi ila wanajeshi wote wa Ukraine wakiweka silaha chini wataweza kuondoka kwa usalama katika eneo la mapigano.






