Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, wakati wa kikao na watumishi wa TFS kilichofanyika wilayani Manyoni mkoani Singida.
"Wajibu wenu ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi ili jamii ielewe na muwe na programu zinazooneshwa kwenye luninga kuelimisha jamii, pia mhakikishe asilimia kubwa ya wawekezaji kwenye miradi ya ufugaji nyuki wawe ni wananchi wa kawaida ili kuwafanya wasikate miti," amesema Masanja.
Aidha, amewataka wahifadhi kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi kuanzia ngazi ya uongozi wa wilaya na mkoa hasa wakati wa ufunguzi wa mashamba ili kuwepo na uhifadhi endelevu.
Naye, Mhifadhi Mkuu Shamba la Nyuki Manyoni, Hashimu Gau, amesema madhumuni ya kuanzisha hifadhi hiyo ni kulinda ikolojia ya Itigi ambayo ni maarufu kwa kuzalisha mazalia ya nyuki, eneo hilo pia hutumiwa na jamii kwa kutundika mizinga yao hivyo kujipatia kipato na ajira za muda mfupi za usafishaji mipaka ulinzi na usafi wa mizinga.
