Jumatatu , 21st Nov , 2016

Mchango wa sekta ya kilimo kwenye uchumi unaweza kuongezeka kutoka kiwango cha sasa cha asilimia thelathini iwapo Tanzania kama nchi itakuwa na mifumo ya kisasa ya ukusanyaji takwimu za kilimo na mifugo.

Katibu Mku Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka

 

Katibu Mku Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt Florence Turuka, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliowakutanisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 25 za Kiafrika, wanaojadili ukusanyaji takwimu za kilimo na mifugo kwa lengo la kusaidia maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao.

Kwa mujibu wa Dkt. Turuka, mifumo bora ya ukusanyaji takwimu itaisaidia serikali kuja na mipango sahihi ya maendeleo ya sekta hiyo hasa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya nusu ya watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi nchini wamejiajiri na baadhi maisha yao yanategemea katika kilimo.