Pamoja na waathiriwa hao watatu, polisi walisema mshukiwa alifariki kutokana na "jeraha la risasi aliyojipiga mwenyewe’’
Watu wengine watano walijeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea katika kampasi kuu ya mji wa Lansing Mashariki jumatatu jioni.
Polisi walimtaja mshukiwa huyo kama "mwanamume mweusi, mfupi kwa kimo". Baadaye walisema alikuwa na umri wa miaka 43 bila uhusiano wowote na chuo kikuu.
Wanafunzi na wakazi wa eneo hilo waliambiwa wakae kwenye majimba yao wakati msako ukiendelea ,hata hivyo polisi baadaye waliondoa agizo hilo, wakisema "hakuna tishio tena chuoni hapo".
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, polisi walisema uchunguzi wao unaendelea., huku nia ya mshambuliaji huyo ikiwa haijulikani.

