Jumatatu , 4th Jan , 2016

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa amewataka watendaji wa shirikla la reli nchini na kampuni hodhi ya mali za reli kuhakikisha sehemu ya reli iliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro inaungwanishwa

Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akifafanua jambo wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo

Prof. Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua athari za mafuriko katika reli hiyo kutoka Kilosa hadi Maguru Kidete kuona athari zilizosababishwa na mvua zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma.

Prof. Mbarawa amesema reli hiyi itaanza kujengwa kuanzia Kesho na amewataka wajenzi hao watumie usiku na mchana ili kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa siku tatu huku wakitakiwa kutafuta suluhu ya kudumu ya kukomesha kuathirika kwa reli hiyo na mafuriko mara kwa mara.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw. Mohammed Selemani Mbunda amemuhakikishia waziri Mbarawa kuwa wananchi wake watashirikiana na serikali katika ujenzi huo na kutafuta suluhu ya kudumu kudhibiti mafuriko yanayoharibu miundo mbinu ya reli katika eneo hilo.

Diwani huyo ameongeza kuwa licha ya mvua hizo kuharibu miundo mbinu hiyo ya reli lakini pia zimeharibu mashamba na kufanya wakazi wa eneo hilo kukabiliwa na baa la njaa kutoka na mazao kuharibiwa yakiwa mashamba