Alhamisi , 26th Mei , 2022

Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Tanzania Sisty Nyahoza amesema kuwa baada ya kumuandikia barua James Mbatia na kumjulisha kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho hatua inayofuata sasa ni kuondoa jina lake kama moja ya viongozi wa Chama

Kiongozi huyo amesema nafasi yake itakaimisha kwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar .

Nyahoza akizungumza na earadio amesisitiza kuwa utaratibu wa kumuondoa kiongozi huyo ulifuata taratibu zote na uamuzi ulikuwa halali

"Sisi baada ya kuwaandikia barua NCCR - Mageuzi kinachofuata sasa ni kusajili mabadiliko ya Uongozi, ndio Sheria inavyosema, kwahiyo sasa hivi tunaweka pembeni jina la Mbatia na nafasi yake anakaimu yule Makamu Mwenyekiti Zanzibar" 

Kuhusu tuhuma alizotoa James Mbatia jana kuwa Ofisi ya Msajili imeshiriki kufadhili mkutano uliomuondoa madarakani, kiongozi huyo amekana tuhuma hizo na kusisitiza ofisi ya msajili haihusiki na hilo 

"Sio kazi ya Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kugharamia mikutano ya vyama, sisi tulialikwa tu,  mbona tulialikwa vya CHADEMA hawasemi tulifadhili, NCCR - Mageuzi wana matatizo yao ndani ya chama wasituletee sisi, kama wana shida zao sisi kazi yetu ni kuangalia nani yupo kwa mujibu wa sheria" amesema Nyahoza

"Sisi tumesema ule mkutano ulikuwa sahihi na Mbatia ameondolewa kihalali, ndio jambo la msingi akae pembeni, mtu ukiona kabisa wenzako hawakutaki ndani ya Chama shida yako nini?, anaongea na vyombo vya habari badala ya kuja Ofisi ya Msajili, tunamkaribisha sana hata leo aje"

"Vyama vya siasa viheshimu Sheria na Katiba zao, vina migogoro mingi kwa sababu wanabishana sana kugombea madaraka, wanakuwa na tamaa ya mali, kama NCCR - Mageuzi walikuwa na masuala ya migogoro ya mali za chama, mambo yameanza siku nyingi na sio sisi tuliyapeleka huko ni wao wenyewe walianzana huko" 

"Sisi baada ya kuwaandikia barua NCCR - Mageuzi kinachofuata sasa ni kusajili mabadiliko ya Uongozi, ndio Sheria inavyosema, kwahiyo sasa hivi tunaweka pembeni jina la Mbatia na nafasi yake anakaimu yule Makamu Mwenyekiti Zanzibar" ameeleza Sisty Nyahoza , Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa